Wednesday, November 21, 2018

Marekani Kwanza, Asema Rais Donald Trump


Saudi ni washiriki muhimu kwa Marekani asema Rais Trump. 

Washington, US 21/11/2018. Rasi wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa, yeye jukumu lake ni kuangalia na kulinda maslahi ya Marekani na siyo suala lake kuingilia masuala ya mambo ya ndani ya matifa mengine.

Rais, Trump alisema hayo wakati alipokuwa akijibu swali kuhusu  Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na ambaye ni raia wa Saud,  na aliye uwawa nchini Uturuki katika ofisi za kibalozi  za Saud Arabia katika jiji la Instabul.

"Marekani ni mshirika na rafiki wa Wasuud Arabia, na tutaendelea kuwa marafiki, kwani tunashirikiana katika nyanja za kiuchumi na ulinzi nakadharika.

"Hivyo tukiwaacha, basi Watafanya biashara na Wachina na Urusi na hata kwingine. Inawezekana kunaukweli hau pia hakuna ukweli kuhusu kuhusika kwa uongozi wa juu wa Saud Arabia katika kifo cha Khashoggi. Ila hilo ni suala la mambo ya ndani ya Wasaud Arabia. Mimi kazi yangu ni kulinda na kungalia maslahi ya Marekani tu" Alisema Rais Trump.

Serikali ya rais Trump imekuwa ililalamikiwa sana, kwa kulifumbia macho hili suala la mauaji ya Khashoggi ambalo linasadikika kuwa amri ya mauaji ilitolewa moja kwa moja na Uongozi wa Kifalme wa Saud. Jambo ambalo serikali ya Saud Arabia imelikataa toka mwanzo.