Thursday, May 16, 2019

Serikali za nchi ruksa kudhibiti matumizi mabaya ya mtandao.

Facebook yakubali serikali kuweka sheria ya kuchunguza wateja wake.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mtandao mkubwa duniani ya Facebook, Mark Zuckerberg, amekubali kuwa serikali zinaweza chunguza na kuzuia wateja wake ambao watakuwa wanaandika au kuweka picha zinazo hashiria uharibifu wa amani katika jamii.

Kukubali huko, kumekuja baada ya Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern's kutaka kuwepo na mkakati wakuzitoa na kuwazuia watu wote wanao tumia vibaya mitandao ya kijamii.  "Inatakiwa hatua za haraka zichukuliwe ili kuondoa mara moja na kuzuia habari na picha zinazo leta uvurugaji wa amani katika jamii ambazo zipo au zitawekwa kwenye mitandao ya kijamii." Alisisitiza Waziri Mkuu Jacinda.

Waziri Mkuu Jacinda, alisema hayo , baada ya kujulikana ya kuwa mtu aliyefanya mashambuli nchi mwake New Zealand, aliutumia mitandao tofauti ya kijamii, na hasa facebook kutangaza unyama aliyoufanya wa kushambulia watu waliokuwa wanaswali msikiti katika mji wa Christchurch.

Mark Zuckerberg alisema " kiukweli ni kwamba sisi tunapinga kiandikwacho au kuwekwacho kenye mtandao ikiwa kinahatarisha maisha au kukuza uasi kwa jamii, hivyo ni ruksa kwa serikali kuweka sheria ambayo itakataza wateja wa facebook kutumia mtandao vibaya."

Mkurugenzimkuu wa facebook amekumbwa na maswali ya uwajibikaji kwa kampuni yake, baada ya baadhi ya wateja wake kubainika kuutumia vibaya mtandao wa facebook katika kutangaza uvunjaji wa amani ndani jamini.

Mark Zuckerberg ambaye ni moja ya waanzilishi wa mtandao huo, amekuwa akikabiliwa na mswali mengi ya kujibu kuhusu mtandao wa kampuni yake katika kuhusika na kukuza maasi kwa jamii, jambo ambalo amekuwa akisema kuwa kampuni ya facebook inapinga vitendo hivyo na ipo tiyari kushirikiana kutokomeza hali hiyo.

No comments:

Post a Comment