Thursday, May 16, 2019

Serikali za nchi ruksa kudhibiti matumizi mabaya ya mtandao.

Facebook yakubali serikali kuweka sheria ya kuchunguza wateja wake.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mtandao mkubwa duniani ya Facebook, Mark Zuckerberg, amekubali kuwa serikali zinaweza chunguza na kuzuia wateja wake ambao watakuwa wanaandika au kuweka picha zinazo hashiria uharibifu wa amani katika jamii.

Kukubali huko, kumekuja baada ya Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern's kutaka kuwepo na mkakati wakuzitoa na kuwazuia watu wote wanao tumia vibaya mitandao ya kijamii.  "Inatakiwa hatua za haraka zichukuliwe ili kuondoa mara moja na kuzuia habari na picha zinazo leta uvurugaji wa amani katika jamii ambazo zipo au zitawekwa kwenye mitandao ya kijamii." Alisisitiza Waziri Mkuu Jacinda.

Waziri Mkuu Jacinda, alisema hayo , baada ya kujulikana ya kuwa mtu aliyefanya mashambuli nchi mwake New Zealand, aliutumia mitandao tofauti ya kijamii, na hasa facebook kutangaza unyama aliyoufanya wa kushambulia watu waliokuwa wanaswali msikiti katika mji wa Christchurch.

Mark Zuckerberg alisema " kiukweli ni kwamba sisi tunapinga kiandikwacho au kuwekwacho kenye mtandao ikiwa kinahatarisha maisha au kukuza uasi kwa jamii, hivyo ni ruksa kwa serikali kuweka sheria ambayo itakataza wateja wa facebook kutumia mtandao vibaya."

Mkurugenzimkuu wa facebook amekumbwa na maswali ya uwajibikaji kwa kampuni yake, baada ya baadhi ya wateja wake kubainika kuutumia vibaya mtandao wa facebook katika kutangaza uvunjaji wa amani ndani jamini.

Mark Zuckerberg ambaye ni moja ya waanzilishi wa mtandao huo, amekuwa akikabiliwa na mswali mengi ya kujibu kuhusu mtandao wa kampuni yake katika kuhusika na kukuza maasi kwa jamii, jambo ambalo amekuwa akisema kuwa kampuni ya facebook inapinga vitendo hivyo na ipo tiyari kushirikiana kutokomeza hali hiyo.

Tuesday, May 14, 2019

China na Marekani (US) zatangaziana jino kwa jino.

China yaweka ngumu kwa bidhaa za Marekani (US).

Serikali ya Uchina imetangaza kupandisha kodi kwa vitu vyote vinavyo ingizwa nchini  China kutoka Marekani kuanzia tarehe 1 Juni 2019, na mbavyo vitagharimu kaisi cha dola za Kimareani $60billion. Mazao ya pamba, vifaa vya ufundi na vifaa vya kutengenezea ndege ndivyo vitakumbwa na kodi hiyo, na wakati huo huo zaidi ya bidhaa 4,000 za Kimarekani zatapandishiwa kodi kufikia 25% kulinganishwa na kodi ya mwanzo ya 10% iliyo kuwa ikitozwa toka mwezi Septemba mwaka 2018.


Uamuzi wa China kupandisha kodi kwa bidhaa za Marekani, nikujibu kitendo kilicho fanywa na serikali ya rais Trump cha kupandisha kodi kwa bidhaa za China zinazo ingizwa nchini Marekani kutoka 10% hadi kufikia 25% ambazo thamani yake ni dola za Kimarekani $200billion.

Kupandishiana kodi kwa Marekani na China, kumeamuliwa na uongozi wa kila nchini, baada ya mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili kushindwa kufikia muafaka ni kwa jinsi gani biashara iendelee bila kuleta hasara katika makampuni ya nchi zao.

Uamuzi wa China na Marekani wa jino kwa jino, linatafsiliwa kuwa ni kitendo cha kulinda bishara na uchumi wa nchi zao. Hata hivyo, Larry Kudlow, mshauri wa masuala ya kiuchumi ya Ikulu ya Marekani alisema kuwa, huenda rais Trump atakutana na rais wa China Xi wakati wa kikao cha G-20 kitakachofanyika Osaka Japani mwezi Juni 2019.  Naye, Liu He, mshauri mkuu wa biashara wa China, amesema kuwa, huenda mkutano mwingine wa majadiliano ya kibiashara ukafanyika Beijing siku za mbele zijazo.


Suala la Marekani na China kuvutana kibiashara lilianza mwaka jana Julai, na tangu hapo nchi zote mbili zimekuwa zikilumbana kibiashara, jambo ambalo limesababisha ugumu wa kibiashara na kuleta hasara kwenye makampuni ya nchi zote mbili,  na pia kufanya ukuaji wa kiuchumi wa mataifa  hayo na ulimwengu wote kuwa wa taratibu.








Monday, May 13, 2019

India yataka mikataba ya biashara ya nchi zinazoendelea iangaliwe upya.

Mtaalmu wa mambo ya uzamiaji Baharini akuta mifuko ya plastiki katika kina kirefu baharini.


Victor Vescovo ambaye ni mmoja wa wataalamu wa kuzamia maji yenye vina virefu duniani, amestajabishwa na wingi wa mifuko ya plastiki aliyokutuna nayo wakati akizamia katika bahari ya Pacific kwenye mkondo wa Marina.

Akiwa amevunja rekodi ya kuzama chini zaidi umbaliwa kilometa 11, Vescovo alisema " nimeona maumbile tofauti ya miamba huko bahari, lakini kilichonishangaza ni kukuta pia mifuko ya plastiki na aina zote zinazo husiana na maplastiki."

Pia nimekuta na kuona aina tofauti ya samaki na viumbe wengine ambayo sidhani kama tulisha wahi kuwaona na wao sidhani walishawahi kutoka katika maeneo walipo, mfano " niliona  kiumbe kama amphipodos nilipo fika mita 7000, lakini nilipo fika mita 8000 hapo ndipo maajabu  ya kuona viumbe tofauti yalizidi." Aliongezea Vescovo.


Wataalamu wa mazingira wamedai kuwa kutokana na alichoona Victor Vescovo, imedhihirisha kuwa vitu vya aina ya plastiki vilikuwa ni hatari kwa mazingira yote, siyo tu kwa binadamu bali pia kwa viumbe wengine hasa waishio baharini na maziwani.

Kina cha bahari ya Marina kinasadikiwa kuwa naurefu  wa zaidi ya mita 11,000, kulinganisha na urefu wa Everest ambao ni mlima mferu duniani wenye mita zipatazo 8,848.

Mpaka sasa, ni watu watatu waliofanikiwa kuzamia kina hiki cha Marina kwa urefu tofauti tangu mwaka 1960 na Victor Vescovo ameweka historia ya pekee yake ya kuzamia kina kirefu zaidi kuliko wazamiaji wa awali wote.

 Msuguano wa biashara za Kimataifa kuingia hatua mpya.

China na Afrika ya Kusini zimethibitisha kuunga mkono ombi la India la kutaka nchi zinazoendelea zilindwe kibiashara jambo ambalo US-Marekani imekuwa ikilipinga.

Kwa mujibu wa habari zilizo chapishwa katika jarida la Econimic Times -Jarida la Biashara na Uchumi wa Kimataifa liripoti  "Afrika ya Kusini na China zimeshakubaliana na ombi la India la kutaka suala la biashara za nchi zinazo endelea kubadirishiwa muundo wake wote," na hivyo kuhaidi  kulipitisha ili liendane na sheria za shirika la biashara la ulimwengu World Trade Organization (WTO).

Ombi la India ni limeandikwa kwamba " nchi zinazo endelea ni lazima zipewe fursa ya kibiashara ya muda mrefu na kupunguziwa kodi katika utendaji wake wa biashara kimataifa ilikuweza kujiendeleza kibiashara ambapo zitaweza fikia uwezo wa nchi zilizo endelea."

Pia ripoti ya India imesisitiza "tunataka pia suala la kuchagua uongozi wa WTO ubadirike. Liripoti jalida la habari la Biashara na Uchumi wa Kimataifa.

India imesha andaa mkatati wakutaka sheria hii iongezwe na itawakilisha ombi hilo katika kikao cha mawaziri wa bishara kitakachofanyika jijini Dheli wiki hii, na kikao hicho kitachukua siku mbili.


Hata hivyo, serkali ya Marekani, imeonekana kutopendezewa na ombi hilo, na wachunguzi wa masuala ya kibiashara na uchumi wamesema kuwa kufuatia hisia hizo za kutoka ikulu ya Marekani, "mgogora wa kibiashara huenda uzuka kati ya nchi zinazo endelea na washiriki wanaounga mkono kwa kupinga ombi la India." Iliripotiwa pia

Mkakati wa ombi la India umewekwa mezani kwa mawaziri wa biashara 14, ili kujadiliwa na kupatiwa jibu haraka, kabla ya mkutano wa G-20 ambao unatarajiwa kufanyika Osaka, nchini Japani mwezi wa Juni mwaka huu.

Saturday, May 11, 2019


CIA ilimwajiri mkuu wa Usalama wa Venezuela.

Aliyekuwa mkuu wa usalama wa Venezulea Christopher Figuera na ambaye inaaminika kuwa alioongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyo shindwa kuiondoa serikali ya Venezuela inayo ongozwa na rais Nicolas Maduro, alikuwa ni mwajiriwa wa shirika la kijasusi la Marekani-CIA.

Akilihutubia taifa, rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema,  Christopher Figuera aliajiriwa na CIA, "na alikuwa msaliti mkuu," na niliaambiwa mapema kuhusu mwenenendo wake, "ila ilibidi tuone mwisho wake ni nini "Na cha kushangaza ni kwamba serikali ya Marekani ilimwondolea vikwazo vya ainazote." Alisisitiza rais Maduro.

Serikali ya Marekani, imewawekea vikwazo vya usafiri na kuzuia mali za baadhi ya watu wapatao 150 toka Venezuela ambapo kuna wafanya biashara, wanasiasa  na wanajeshi pia.

Wakati huo huo, makamu wa rais wa bunge la Venezuela Edger Zambrono amekamatwa baada ya kujulikana kuwa alikuwa ni mmoja wa viongozi walio ongoza jaribio lililoshindwa la kuingusha serikali ya rais Maduro.

Veneluela imekuwa ikipinga kitendo cha Marekani kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, nakutokana na hali hii kuwepo, mahusiano ya nchi hizi mbili yamedorola kwa kiasi kikubwa katika nyanja zote zinazohusu mahusiano ya nchi na nchi.

Chama cha ANC cha shinda  tena uchaguzi mkuu nchini Afrika ya Kusini .

Chama cha  African National Congress (ANC) nchini Afrika ya Kusini kimeshinda tena uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao ulifanyika siku ya Jumatano wiki hii kwa kuibuka na ushindi wa alisimia 57.51%, japokuwa matokeo ya ushindi huu ni yachini kulinganishwa na ushindi ambao imekuwa ikiupata katika uchaguzi wa miaka ya nyuma.


Ushindi huu, umemwezesha rais Cyril Ramaphosa kuunda serikali itakayo ongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya Wapiga kura kukipa ANC wingi wa wabunge ambao watawawakilisha.

Vyama vingene ambavyo vilishiriki katika uchaguzi huu mkuu ni Democratic Alliance (DA) kilichopata alimia 20.76% na Economic Freedom Fighter (EFF) kilipata asilimia 10.79%.

" Rais Ramaphosa anakazi ngumu ya kutatua suala la ardhi nchini mwetu, ambapo hadi sasa inashikiliwa na watu wachache, na ikiweza kulitatua hilo jambo, basi atakuwa ametimiza moja ya ahadi ya chama chake cha ANC kwa wananchi." Alisema  Dr Philip Siphiwe.

Rais Ramaphosa, alichukua uongozi toka mikononi mwa rais Jacob Zuma mwaka 2018 Februari, nahivyo ushindi huu  ambao ummempa madaraka kamili utakuwa ni kipomo cha ahadi yake ya kujenga uchumi wa nchi utakao inuwa kipato cha wananchi hasa Waafrika weusi ambao wengi bado wanaishi maisha duni.


Friday, May 10, 2019

Wapalestina walia na Trump

Wapalestina Walia na Uongozi wa Trump

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina, Riyad al Maliki amesema kuwa suala la kuwepo kwa amani kati ya Wapalestina ana Waizrael linavurugwa na serikali ya Marekani.

"Kiukweli kuwa na imani na uongozi wa sasa wa Marekani ni vigumu sana," kwani serikali ya inayoongozwa na rais Trump "imeshaandika hukumu ya  kujitole kwa Wapalestina kwa Waizrael" alisema waziri Maliki.

Waziri Maliki, aliyasema hayo wakati alipokuwa amekutana na mshauri wa masuala ya amani ya Waizrael na Wapalestina wakati walipo kutana katika ofisi za makao makuu ya umoja wa Mataifa jijini New York hivi karibuni kujadili nini kifanyike ili kuleta amani ya kudumu.

Katika mkutano huo, Waziri Maliki alisisitiza kuwa kitendo cha uongozi wa Marekani ulipo chini ya rais Trump kukubali kwa kuunga mkono kuwa Jerusalem kuwa makao makuu ya Izrael, kumetoa picha kamili ya kutokuwa na imani na serikali ya sasa ya Marekani.

"Mgogoro kati ya Izreal na Palestina umekuwa mthiani ambao upande mmoja umekuwa ukipendelewa." Aliongea Maliki, akimaanisha kuwa Uongozi wa Marekani umekuwa ukifumbia macho vitendo vinavyo fanywa na Izrael kwa Wapalestina.

Hata hivyo katika mazungumzo hayo, Waziri Maliki alisisitiza kuwa Wapalestina wataendelea kuunga mkono masuala yote yatakayo saidia kuleta amani ya kudumu kati ya Wapalestina na Waizrael.

Kwa mujibu wa habari kutoka katika mkutano huo, rasimu ya kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina inatarajiwa kuchapishwa baada ya mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani kuisha.


Shirika la Afya Ulimwengu WHO bado kupata jibu la kudumu la ugonjwa wa Dengue.


Habari kutoka shirika la Afya Ulimwenguni, zinamsema kuwa, bado halijapata jibu kamili la kupambana na ugonjwa wa Dengue ambao umekuwa ni tishio katika maisha ya watu duniani.


Ugonjwa wa Dengue umekuwa ukisambaa kwa haraka katika nchi zinazoendelea ambazo zipo katika bara la Afrika, Nchi za Amerika, Mashariki ya Mediteranian, Kusini Asia na nchi zilizopo Magahribi ya Pasifiki

"Ugonjwa huu, ambao unasemekana kusambaa kwa kwasi duniani na kuathiri mamilioni ya watu, umekuwa hautambulishwi kuwa ugonjwa hatari kama magonjwa mengine makuu japokuwa unasambaa kwa haraka na kuhatarisha maisha ya watu kila siku." Iliieza WHO report.

Uenezaji wa habari wa athari za ugonjwa wa Dengue "umekuwa ukiripotiwa chini ya kiwango kulinganisha na idadi ya watu walioathirika jambo ambalo linaaleta utata katika kujua ukweli wa athali za ugonjwa huu katika jamii nzima ya kimataifa", ilisisitiza ripoti ya WHO.

Hadi sasa  watu wapatao 390 million wamesha ambukizwa na vidudu vya ugonjwa huu katika nchi 128 duniani na idadi hii huenda ikaongezeka kwa haraka zaidi, kwani tangu mwaka 2010  idadi ya watu walioambukiwa na ugonjwa huu  was Dengue ilipanda toka 2.2 million na kufikia 3.34 million mwaka 2016.

Hata hivyo ripoti ya WHO, imesema kuna dawa aina ya Dengvaxia(CYD-TDV) ambayo kwa sasa inasaidia kutibu ugonjwa huu kutegemea ni kwa kiasi gani mtu ameathirika na ugonjwa huu.

Ugonjwa wa Dengue, ulianza julikana kabla ya mwaka 1970, na ni nchi 9 duniani ziliathirika na ugonjwa huu, lakini idai imezidi ongezeka kwa kwasi zaidi na kufikia nchi 100 ambazo zimesha kumbwa na ugonjwa huu.  Dengue ni ugonjwa unaombukizwa na mbu wa kike wajulikanao kama Aedes eagypti na Ae albopicus ambao hubeba virusi vya ugonjwa huu.



















 








Wednesday, May 8, 2019

Visu vyatishia maisha ya watu jijini London

Matumizi ya visu kudhuru watu katika jiji la London waongezeka.

Ripoti ya Polisi kuhusu matumizi ya visu kama nyenzo ya kudhuria watu yamekuwa makubwa nchi Uingereza tangu mwaka 1946, na Jiji la London  linaongoza kwa matumizi ya visu kama siraha na tangu mwaka uanze wa 2019 hadi kufikia tarehe 27 April, 2019, watu wapatao 27 walipoteza maisha.

Kwa mujibu wa  ripoti, Jiji la London, limekuwa likiongoza katika matumizi ya visu kudhuru watu na kati ya watu 100,000 katika mwaka 2017-18, watu 168 walichomwa na visu na kupoteza maisha.



Ongezeko la matumizi ya visu limeongezeka katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ambayo imeishia mwezi wa Septemba 2018, kwa kesi zinazohusha matumizi ya visu kuwa 39,818.

Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi, wengi waanaodhurika na kuhusika na matumizi ya visu ni vijana wa Kiafrika na wenye asili ya Kiashia ambao ongezeko lao limefikia 25% kitaifa.


Akiongela kuhusu suala zima la matumizi ya visu kama siraha jijini,  mkuu wa Jeshi la Polisi London Cressida Dick amesema " jeshi la polisi linafanya kila  jitihada kupambana na hali hii ya matumizi ya visu katika jiji la London."

Hata hivyo suala la polisi kupambana na matumizi ya visu limekuwa likikutwa na vikwazo vya kisiasa kwa madai polisi wanachagua watu wasio wazungu kuwakagua na kuwaacha wazungu.


Rais wa Iran atangaza kuwa nchi yake kuendelea kuzalisha virutubisho ya Nuklia.

Rais wa Iran, Hassan Rouhania ametangaza kuwa Iran itaanza kuzalisha virutubisho ninavyo zalisha Nuklia, ikiwa nchi za jumuya ya Ulaya hazitaeleza msimamo wao juu ya suala hilo.

Akitangaza kwa Taifa la Iran, rais Rouhania alisema, Iran itasimamisha mikataba yote iliyo sainiwa kati ya Iran na nchi za EU, ikiwa  urahisi wa vikwazo vya kiuchumi zidi ya Iran utaondolewa kama "Marekani inavyotaka."

Mkataba wa kurahisisha vikwazo kwa Iran,  ulisainiwa miaka minne iliyo pita na unajulikana kama P5+1
Joint Comprehensive Plan of Action ambao (JCPOA) na nchi zilizo shiriki ni  Marekani Uingereza, France, China, Urussi, Ujerumani and Umoja wa Ulaya.


Mbunge wa Marekani aumana vichwa na serikali kuhusu Venezuela.

Ilhan Omar, Mbunge wa Kongresi wa chama cha Demokrati nchini Marekani, amepingana vikali na makamu wa rais Mike Pence kuhusu hali ilivyo Venezuela na ushiriki wa Marekani katika nchi hiyo.

Akiongea Makamu wa Rais Pence amesema, Ilhan ni muumini wa ujamaa"anaye pingana na demokrasia na uhuru wa watu kutaka mabadiriko." Naye Ilhan Omar ambaye ni mbuge kutoka chama cha Demokratiki amesema,  imekuwa ni kawaida "mtu akipinga vitendo visivyo halali vinavyo fanywa na Marekani kuitwa "mpinzani wa demokrasi." Na ukweli ulijieleza wakati wa "vita vya Irak" aliongezea  Ilhan.

Mvutano huu, umekuja baada ya serikali ya Marekani inayo ongozwa na rais Trump na cham cha Republikani kutamka kuwa kinamuunga mkono Juan Guaido, mpizani wa serikali ya Venezulea, na ambaye alijitangazia urais na pia kushutumiwa kwa kuongoza mapindizi ya kijeshi zidi serikali hivi karibuni.

Tuesday, May 7, 2019

Marekani kupeleka ndege za kivita 4B-52 Mashariki ya Kati.

Katika harakati za kujiweka imara kiulinzi, Marekani inapangakupeleka ndege za  kivita aina 4B-52, huko Mashariki ya Kati, kitendo kinacho sadikiwa kuwa ni kujitaadhari na mashambulizi toka Iran.

Habari kutoka Pentagon- makao makuu ya usalama wa Marekani, zinasema ndege hizo zipo tiyari kuondoka kuelekea nchi Katar muda wowote wiki hii.


Akiongea kuhusu kupelekwa kwa ndege hizo, mshauri wa masuala ya kiulinzi na usalama wa Marekani, John Bolton amesema, " Marekani imefanya uamuzi huo kutokana na uhalisia wa hali iliyopo katika eneo hilo, na hasa Iran kuonyesha dalili za kujiandaa kivita."

Ndege hizo za kivita zitaondoka katika kutuo cha kijeshi cha ndege kilichopo Louisian nchini Marekani.
Kupangwa kuondoka kwa ndege hizo, kunakuja baada ya melikebu ya kivita ya Makereni kwa jina Abraham Lincoln kuondoka hivi karibuni kuelekea kwenye bahari iliyopo Mashariki ya Kati.