Waziri wa mambo ya nje wa Palestina, Riyad al Maliki amesema kuwa suala la kuwepo kwa amani kati ya Wapalestina ana Waizrael linavurugwa na serikali ya Marekani.
"Kiukweli kuwa na imani na uongozi wa sasa wa Marekani ni vigumu sana," kwani serikali ya inayoongozwa na rais Trump "imeshaandika hukumu ya kujitole kwa Wapalestina kwa Waizrael" alisema waziri Maliki.
Waziri Maliki, aliyasema hayo wakati alipokuwa amekutana na mshauri wa masuala ya amani ya Waizrael na Wapalestina wakati walipo kutana katika ofisi za makao makuu ya umoja wa Mataifa jijini New York hivi karibuni kujadili nini kifanyike ili kuleta amani ya kudumu.
"Mgogoro kati ya Izreal na Palestina umekuwa mthiani ambao upande mmoja umekuwa ukipendelewa." Aliongea Maliki, akimaanisha kuwa Uongozi wa Marekani umekuwa ukifumbia macho vitendo vinavyo fanywa na Izrael kwa Wapalestina.
Hata hivyo katika mazungumzo hayo, Waziri Maliki alisisitiza kuwa Wapalestina wataendelea kuunga mkono masuala yote yatakayo saidia kuleta amani ya kudumu kati ya Wapalestina na Waizrael.
Kwa mujibu wa habari kutoka katika mkutano huo, rasimu ya kuleta amani kati ya Waizrael na Wapalestina inatarajiwa kuchapishwa baada ya mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani kuisha.
Shirika la Afya Ulimwengu WHO bado kupata jibu la kudumu la ugonjwa wa Dengue.
Habari kutoka shirika la Afya Ulimwenguni, zinamsema kuwa, bado halijapata jibu kamili la kupambana na ugonjwa wa Dengue ambao umekuwa ni tishio katika maisha ya watu duniani.
Ugonjwa wa Dengue umekuwa ukisambaa kwa haraka katika nchi zinazoendelea ambazo zipo katika bara la Afrika, Nchi za Amerika, Mashariki ya Mediteranian, Kusini Asia na nchi zilizopo Magahribi ya Pasifiki
"Ugonjwa huu, ambao unasemekana kusambaa kwa kwasi duniani na kuathiri mamilioni ya watu, umekuwa hautambulishwi kuwa ugonjwa hatari kama magonjwa mengine makuu japokuwa unasambaa kwa haraka na kuhatarisha maisha ya watu kila siku." Iliieza WHO report.
Uenezaji wa habari wa athari za ugonjwa wa Dengue "umekuwa ukiripotiwa chini ya kiwango kulinganisha na idadi ya watu walioathirika jambo ambalo linaaleta utata katika kujua ukweli wa athali za ugonjwa huu katika jamii nzima ya kimataifa", ilisisitiza ripoti ya WHO.
Hadi sasa watu wapatao 390 million wamesha ambukizwa na vidudu vya ugonjwa huu katika nchi 128 duniani na idadi hii huenda ikaongezeka kwa haraka zaidi, kwani tangu mwaka 2010 idadi ya watu walioambukiwa na ugonjwa huu was Dengue ilipanda toka 2.2 million na kufikia 3.34 million mwaka 2016.
Hata hivyo ripoti ya WHO, imesema kuna dawa aina ya Dengvaxia(CYD-TDV) ambayo kwa sasa inasaidia kutibu ugonjwa huu kutegemea ni kwa kiasi gani mtu ameathirika na ugonjwa huu.
Ugonjwa wa Dengue, ulianza julikana kabla ya mwaka 1970, na ni nchi 9 duniani ziliathirika na ugonjwa huu, lakini idai imezidi ongezeka kwa kwasi zaidi na kufikia nchi 100 ambazo zimesha kumbwa na ugonjwa huu. Dengue ni ugonjwa unaombukizwa na mbu wa kike wajulikanao kama Aedes eagypti na Ae albopicus ambao hubeba virusi vya ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment