Saturday, May 11, 2019


CIA ilimwajiri mkuu wa Usalama wa Venezuela.

Aliyekuwa mkuu wa usalama wa Venezulea Christopher Figuera na ambaye inaaminika kuwa alioongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyo shindwa kuiondoa serikali ya Venezuela inayo ongozwa na rais Nicolas Maduro, alikuwa ni mwajiriwa wa shirika la kijasusi la Marekani-CIA.

Akilihutubia taifa, rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema,  Christopher Figuera aliajiriwa na CIA, "na alikuwa msaliti mkuu," na niliaambiwa mapema kuhusu mwenenendo wake, "ila ilibidi tuone mwisho wake ni nini "Na cha kushangaza ni kwamba serikali ya Marekani ilimwondolea vikwazo vya ainazote." Alisisitiza rais Maduro.

Serikali ya Marekani, imewawekea vikwazo vya usafiri na kuzuia mali za baadhi ya watu wapatao 150 toka Venezuela ambapo kuna wafanya biashara, wanasiasa  na wanajeshi pia.

Wakati huo huo, makamu wa rais wa bunge la Venezuela Edger Zambrono amekamatwa baada ya kujulikana kuwa alikuwa ni mmoja wa viongozi walio ongoza jaribio lililoshindwa la kuingusha serikali ya rais Maduro.

Veneluela imekuwa ikipinga kitendo cha Marekani kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo, nakutokana na hali hii kuwepo, mahusiano ya nchi hizi mbili yamedorola kwa kiasi kikubwa katika nyanja zote zinazohusu mahusiano ya nchi na nchi.

Chama cha ANC cha shinda  tena uchaguzi mkuu nchini Afrika ya Kusini .

Chama cha  African National Congress (ANC) nchini Afrika ya Kusini kimeshinda tena uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambao ulifanyika siku ya Jumatano wiki hii kwa kuibuka na ushindi wa alisimia 57.51%, japokuwa matokeo ya ushindi huu ni yachini kulinganishwa na ushindi ambao imekuwa ikiupata katika uchaguzi wa miaka ya nyuma.


Ushindi huu, umemwezesha rais Cyril Ramaphosa kuunda serikali itakayo ongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya Wapiga kura kukipa ANC wingi wa wabunge ambao watawawakilisha.

Vyama vingene ambavyo vilishiriki katika uchaguzi huu mkuu ni Democratic Alliance (DA) kilichopata alimia 20.76% na Economic Freedom Fighter (EFF) kilipata asilimia 10.79%.

" Rais Ramaphosa anakazi ngumu ya kutatua suala la ardhi nchini mwetu, ambapo hadi sasa inashikiliwa na watu wachache, na ikiweza kulitatua hilo jambo, basi atakuwa ametimiza moja ya ahadi ya chama chake cha ANC kwa wananchi." Alisema  Dr Philip Siphiwe.

Rais Ramaphosa, alichukua uongozi toka mikononi mwa rais Jacob Zuma mwaka 2018 Februari, nahivyo ushindi huu  ambao ummempa madaraka kamili utakuwa ni kipomo cha ahadi yake ya kujenga uchumi wa nchi utakao inuwa kipato cha wananchi hasa Waafrika weusi ambao wengi bado wanaishi maisha duni.


No comments:

Post a Comment