Tuesday, May 14, 2019

China na Marekani (US) zatangaziana jino kwa jino.

China yaweka ngumu kwa bidhaa za Marekani (US).

Serikali ya Uchina imetangaza kupandisha kodi kwa vitu vyote vinavyo ingizwa nchini  China kutoka Marekani kuanzia tarehe 1 Juni 2019, na mbavyo vitagharimu kaisi cha dola za Kimareani $60billion. Mazao ya pamba, vifaa vya ufundi na vifaa vya kutengenezea ndege ndivyo vitakumbwa na kodi hiyo, na wakati huo huo zaidi ya bidhaa 4,000 za Kimarekani zatapandishiwa kodi kufikia 25% kulinganishwa na kodi ya mwanzo ya 10% iliyo kuwa ikitozwa toka mwezi Septemba mwaka 2018.


Uamuzi wa China kupandisha kodi kwa bidhaa za Marekani, nikujibu kitendo kilicho fanywa na serikali ya rais Trump cha kupandisha kodi kwa bidhaa za China zinazo ingizwa nchini Marekani kutoka 10% hadi kufikia 25% ambazo thamani yake ni dola za Kimarekani $200billion.

Kupandishiana kodi kwa Marekani na China, kumeamuliwa na uongozi wa kila nchini, baada ya mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili kushindwa kufikia muafaka ni kwa jinsi gani biashara iendelee bila kuleta hasara katika makampuni ya nchi zao.

Uamuzi wa China na Marekani wa jino kwa jino, linatafsiliwa kuwa ni kitendo cha kulinda bishara na uchumi wa nchi zao. Hata hivyo, Larry Kudlow, mshauri wa masuala ya kiuchumi ya Ikulu ya Marekani alisema kuwa, huenda rais Trump atakutana na rais wa China Xi wakati wa kikao cha G-20 kitakachofanyika Osaka Japani mwezi Juni 2019.  Naye, Liu He, mshauri mkuu wa biashara wa China, amesema kuwa, huenda mkutano mwingine wa majadiliano ya kibiashara ukafanyika Beijing siku za mbele zijazo.


Suala la Marekani na China kuvutana kibiashara lilianza mwaka jana Julai, na tangu hapo nchi zote mbili zimekuwa zikilumbana kibiashara, jambo ambalo limesababisha ugumu wa kibiashara na kuleta hasara kwenye makampuni ya nchi zote mbili,  na pia kufanya ukuaji wa kiuchumi wa mataifa  hayo na ulimwengu wote kuwa wa taratibu.








No comments:

Post a Comment