Mtaalmu wa mambo ya uzamiaji Baharini akuta mifuko ya plastiki katika kina kirefu baharini.
Victor Vescovo ambaye ni mmoja wa wataalamu wa kuzamia maji yenye vina virefu duniani, amestajabishwa na wingi wa mifuko ya plastiki aliyokutuna nayo wakati akizamia katika bahari ya Pacific kwenye mkondo wa Marina.
Akiwa amevunja rekodi ya kuzama chini zaidi umbaliwa kilometa 11, Vescovo alisema " nimeona maumbile tofauti ya miamba huko bahari, lakini kilichonishangaza ni kukuta pia mifuko ya plastiki na aina zote zinazo husiana na maplastiki."
Pia nimekuta na kuona aina tofauti ya samaki na viumbe wengine ambayo sidhani kama tulisha wahi kuwaona na wao sidhani walishawahi kutoka katika maeneo walipo, mfano " niliona kiumbe kama amphipodos nilipo fika mita 7000, lakini nilipo fika mita 8000 hapo ndipo maajabu ya kuona viumbe tofauti yalizidi." Aliongezea Vescovo.
Wataalamu wa mazingira wamedai kuwa kutokana na alichoona Victor Vescovo, imedhihirisha kuwa vitu vya aina ya plastiki vilikuwa ni hatari kwa mazingira yote, siyo tu kwa binadamu bali pia kwa viumbe wengine hasa waishio baharini na maziwani.
Kina cha bahari ya Marina kinasadikiwa kuwa naurefu wa zaidi ya mita 11,000, kulinganisha na urefu wa Everest ambao ni mlima mferu duniani wenye mita zipatazo 8,848.
Mpaka sasa, ni watu watatu waliofanikiwa kuzamia kina hiki cha Marina kwa urefu tofauti tangu mwaka 1960 na Victor Vescovo ameweka historia ya pekee yake ya kuzamia kina kirefu zaidi kuliko wazamiaji wa awali wote.
Msuguano wa biashara za Kimataifa kuingia hatua mpya.
China na Afrika ya Kusini zimethibitisha kuunga mkono ombi la India la kutaka nchi zinazoendelea zilindwe kibiashara jambo ambalo US-Marekani imekuwa ikilipinga.
Kwa mujibu wa habari zilizo chapishwa katika jarida la Econimic Times -Jarida la Biashara na Uchumi wa Kimataifa liripoti "Afrika ya Kusini na China zimeshakubaliana na ombi la India la kutaka suala la biashara za nchi zinazo endelea kubadirishiwa muundo wake wote," na hivyo kuhaidi kulipitisha ili liendane na sheria za shirika la biashara la ulimwengu World Trade Organization (WTO).
Ombi la India ni limeandikwa kwamba " nchi zinazo endelea ni lazima zipewe fursa ya kibiashara ya muda mrefu na kupunguziwa kodi katika utendaji wake wa biashara kimataifa ilikuweza kujiendeleza kibiashara ambapo zitaweza fikia uwezo wa nchi zilizo endelea."
Pia ripoti ya India imesisitiza "tunataka pia suala la kuchagua uongozi wa WTO ubadirike. Liripoti jalida la habari la Biashara na Uchumi wa Kimataifa.
India imesha andaa mkatati wakutaka sheria hii iongezwe na itawakilisha ombi hilo katika kikao cha mawaziri wa bishara kitakachofanyika jijini Dheli wiki hii, na kikao hicho kitachukua siku mbili.
Hata hivyo, serkali ya Marekani, imeonekana kutopendezewa na ombi hilo, na wachunguzi wa masuala ya kibiashara na uchumi wamesema kuwa kufuatia hisia hizo za kutoka ikulu ya Marekani, "mgogora wa kibiashara huenda uzuka kati ya nchi zinazo endelea na washiriki wanaounga mkono kwa kupinga ombi la India." Iliripotiwa pia
Mkakati wa ombi la India umewekwa mezani kwa mawaziri wa biashara 14, ili kujadiliwa na kupatiwa jibu haraka, kabla ya mkutano wa G-20 ambao unatarajiwa kufanyika Osaka, nchini Japani mwezi wa Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment